Rais Dkt Mwinyi amejumuika katika futari iliyoandaliwa na Balozi Mdogo wa Oman.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na viongozi mbalimbali katika futari iliyoandaliwa na Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Said Salim Al Sinawi iliyofanyika Hoteli ya Golden Tulip Airport leo tarehe 18 Aprili 2023, Mkoa wa Mjini Magharibi.